1 Samuel 8:1-6

Israeli Waomba Mfalme

1 aSamweli alipokuwa mzee, akaweka wanawe kuwa waamuzi wa Israeli. 2 bMzaliwa wa kwanza alikuwa Yoeli, na la wa pili lilikuwa Abiya, nao wakatumika huko Beer-Sheba. 3 cLakini wanawe hawakuenenda katika njia zake. Waliziacha wakageukia faida za udanganyifu nao wakapokea rushwa na kupotosha haki.

4 dBasi wazee wote wa Israeli wakakusanyika pamoja na kumjia Samweli huko Rama. 5 eWakamwambia, “Wewe umekuwa mzee, nao wanao hawaenendi katika njia zako, sasa tuteulie mfalme wa kutuongoza, kama ilivyo kwa mataifa mengine yote.”

6 fLakini wao waliposema, “Tupe mfalme wa kutuongoza,” hili lilimchukiza Samweli, hivyo akamwomba Bwana.
Copyright information for SwhKC